• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ureno na Ubelgiji zawanyeshea mvua ya magoli wapinzani wao

    (GMT+08:00) 2016-10-11 09:25:14

    Michezo tisa ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 imechezwa barani ulaya ambapo mataifa ya Ubelgiji, Ureno na Ufaransa yameshinda michezo yao. Mashetani wekundu Ubelgiji wakicheza ugenini wamewanyeshea wenyeji wao Gibraltar mvua ya magoli 6-0, mshambuliaji Christian Benteke, amefunga mabao matatu na mabao mengine yakifungwa na Dries Mertens, Eden Hazard na Kiungo Axel Witsel.

    Ureno nao wakawachapa kisiwa cha Faroe, kwa mabao 6-0 Andre Silva, akiibuka shujaa kwa kufunga mabao matatu peke yake. Kwa upande wa Ufaransa wakawatambia Uholanzi nyumbani kwa kuwafunga bao 1-0 bao lililofungwa na mchezaji ghali duniania Paul Pogba. Bosnia -Herzegovina, wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cyprus, Estonia wakiwa nyumbani wamekubali kulala kwa kuchapwa kwa mabao 2-0 na Ugiriki.

    Latvia nao wamefungwa kwa mabao 2-0 na Hungary, Huku Andorra wakishindwa kutamba nyumbani baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Switzerland. Belarus na Luxembourg wametoshana nguvu kwa sare ya goli 1-1, Sweden wakang'ara nyumbani kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bulgaria

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako