• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia na Uturuki zasaini makubaliano ya ujenzi wa mradi wa mabomba ya gesi

    (GMT+08:00) 2016-10-11 10:50:43

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na mwenzake wa Russia Vladimir Putin ambaye yuko ziarani nchini Uturuki, jana huko Istanbul walisaini makubaliano ya ujenzi wa mradi wa mabomba ya gesi asilia.

    Kwenye sherehe ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, rais Erdogan ameeleza imani yake kuwa uhusiano kati ya Uturuki na Russia utaendelea kurudi katika hali ya kawaida.

    Rais Putin ametangaza kuwa Russia imekubali kusafirisha gesi asilia kwa Uturuki kwa bei nafuu, na kuondoa vikwazo vya uagizaji wa matunda kutoka Uturuki. Amesema nchi hizo mbili zitahimiza kurudisha uhusiano wa kawaida kati yao kwenye ushirikiano wa kijeshi, biashara, utalii na utamaduni.

    Baadhi ya mabomba manne yatakayojengwa chini ya mradi huo yanaweza kusafirisha gesi asilia kwa Ulaya ya Mashariki na kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako