• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Bakhresa kujenga viwanda vingine vya matunda

    (GMT+08:00) 2016-10-12 19:37:49

    KAMPUNI ya Bakhresa Foods imedhamiria kuongeza viwanda vingine vya usindikaji matunda nchini ili kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima.

    Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Said Salim Bakhresa ametoa ahadi hiyo wakati alipokutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

    Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bakhresa amesema wana mpango wa kujenga kiwanda kimoja kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watu wanapata usumbufu wa kusafirisha matunda hadi Dar es Salaam ndipo wayauze.

    Amesema wana mpango wa kuendeleza usindikaji wa vyakula vya nafaka kwenye mikoa ya Kusini na kwamba hadi sasa wameajiri wafanyakazi zaidi ya 8,000 wakiwemo Watanzania 180 ambao wameajiriwa kwenye matawi yake nje ya nchi.

    Amesema hivi sasa kampuni hiyo imefungua matawi mengine kwenye nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako