• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Madini hatari zaidi duniani

  (GMT+08:00) 2016-10-13 16:16:21

  Moja kati ya madini hatari zaidi duniani ni Uranium, ambayo yanaweza kutumiwa kutengeneza mabomu ya nyuklia. Lakini unajua madini hayo pia yaliwahi kutumiwa kutengeneza vioo?

  Madini ya Uranium yana sura ya kupendeza sana. Watu wakiona madini hayo, wanaweza kufikiri ni uyoga wa rangi ya kupendeza na wenye sumu, na madini ya uranium yenye sura ya kupendeza hakika yanatoa mionzi ya kutisha.

  Madini ya Uranium kweli yanatoa mionzi, lakini si ya kutisha kama watu wanavyofikiria.

  Utafiti unaonesha kuwa ukichukua kilo moja ya madini hayo mfukoni, mionzi unayopata kila siku ni karibu sawa na kuvaa saa inayong'ara wakati wa usiku. Zamani watu walitumia madini hayo kutia rangi kwenye vyombo vya vioo. Uranium inatoa mionzi wa chembe za alfa. Miongoni mwa mionzi ya alfa, beta na gama, mionzi ya alfa ina uwezo mdogo wa kupenya, na inaweza hata kuzuiliwa na karatasi. Unaweza kuchukua unga wenye asilimia 80 Uranium oxide kwa mikono yako moja kwa moja. Na ukivaa glavu utaweza kuchukua nishati ya nyuklia inayotumiwa kwenye kituo cha kuzalisha umeme.

  Lakini wafanyakazi wanapochimba madini ya Uranium, wanahitaji kuchukua hatua nyingi ili kujikinga na mionzi, unajua kwa nini?

  Kwa sababu madini hayo yamehifadhiwa chini ya ardhi kwa miaka mingi sana, mionzi mingi imejilimbikiza huko. Mionzi hiyo haitolewi moja kwa moja na Uranium, bali inatolewa na hewa ya Radoni ambayo imebadilika kutoka Uranium.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako