• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wafanya biashara wamlilia Magufuli kuhusu tozo mpya za TBS

    (GMT+08:00) 2016-10-13 19:26:25

    Wafanyabiashara ndogo ndogo wa soko la Kariakoo, Dar es Salaam wamemtaka rais John Pombe Magufuli wa Tanzania aingilie tozo mpya zinazotozwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) kwa madai kwamba zinawafilisi.

    Wakizungumza na radio China Kimataifa, wafanyabiashara hao wamedai kwamba kwa takribani wiki moja sasa wameshindwa kutoa hata kontena moja bandarini kwa sababu ya gharama kubwa wanazotozwa.

    TBS imeanzisha utaratibu mpya wa kulipisha faini mizigo inayoingia nchini humo ambayo haikukaguliwa nchini China, faini ambayo ni asilimia 15 ya thamani ya mzigo ulioingia. Kwa kawaida, wafanyabiashara ndogo wa Kariakoo wana mitaji midogo hivyo huagiza mizigo kutoka nje kwa kushirikiana na kuagiza kwa pamoja kwa kutumia kontena moja.

    Hata hivyo kwa mujibu wa taratibu za TBS katika ukaguzi nje ya nchi, mizigo midogo yenye thamani ya chini ya dola 10,000 huwa haikaguliwi lakini inapofika Tanzania na kuonekana haijakaguliwa, wafanyabiashara hao hupigwa faini.

    Kwa sasa, biashara kubwa inayofanyika Kariakoo ni ile ya Watanzania kuagiza bidhaa kutoka China na kuziweka kwenye maduka yao na vifungashio vyao halafu watu wa nchi jirani wanazinunua na kuzipeleka kwao.

    Tanzania hivi sasa inafanya ukaguzi wa bidhaa zote zinazoingia nchini humo ili kudhibiti ubora (pre-shipment inspections).

    Mwanzoni, bidhaa kama magari tu ndizo zilizokuwa zinakaguliwa lakini baadaye serikali ikaona ni bora kukagua bidhaa zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako