• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Venus ni sayari yenye mazingira ya kutisha!

    (GMT+08:00) 2016-10-14 15:24:03

    Sayari ya Venus ipo jirani na dunia yetu. Ukubwa wa sayari hiyo unafanana na dunia, lakini mazingira ni tofauti kabisa, ambayo ni mabaya sana.

    1. Sayari ya Venus ina ugasumaku mdogo kuliko dunia. Ugasumaku usiotosha hauwezi kuzuia mionzi ya anga ya juu kuingia kwenye angahewa, na mionzi hiyo itasababisha umeme kutokea kwenye mawingu.

    2. Venus ina volkeno nyingi zaidi kuliko sayari nyingine yoyote ya mfumo wa jua. Wanajimu wamegundua volkeno 1600 kwenye sayari hiyo.

    3. Venus ikizunguka yenyewe kwa mzunguko mmoja inahitaji siku 243 za dunia yetu, na ikizunguka jua kwa mzunguko mmoja inahitaji siku 224.7 kwenye dunia yetu. Unaona sentensi hii ni vigumu kuelewa? Hii inamaanisha kuwa kwenye sayari hiyo siku moja ni ndefu zaidi kuliko mwaka mmoja!

    4. Asilimia kubwa ya hewa kwenye Venus ni Carbon Dioxide, ambayo inasababisha sayari hiyo iwe na joto kali, ambalo linaweza kufikia nyuzi 470 sentigredi.

    5. Shinikizo la hewa kwenye Venus ni kubwa sana, ambalo ni mara 90 ya lile la dunia yetu, na karibu sawa na shinikizo la maji kwenye kina cha kilomita 1 chini ya bahari.

    6. Venus ni sayari yenye vimbunga vingi. Mwendo kasi wa upepo wa sayari hiyo unaweza kufikia kilomita 724 kwa saa, ambao ni mkubwa zaidi kuliko mwendo kasi wa kimbunga kikubwa zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako