• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wasiopungua 24 wameuawa katika mashambulizi ya kundi la IS huko Kirkuk, Iraq

    (GMT+08:00) 2016-10-21 18:26:11

    Watu wasiopungua 24 wameuawa na wengine 12 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kundi la IS huko Kirkuk, kaskazini mwa Iraq.

    Leo asubuhi wapiganaji kadhaa wa kundi la IS, ambao baadhi yao walikuwa wamevaa mabomu, walishambulia jengo la polisi, majengo mengine ya serikali na misikiti kadhaa mjini Kirkuk, kilomita 250 kaskazini ya mji wa Baghdad.

    Baada ya kupambana vikali na walinzi wa majengo hayo, washambuliaji hao walifanikiwa kutwaa udhibiti wa baadhi ya majengo, ikiwemo makao makuu ya polisi, msikiti mmoja na nyumba moja.

    Shambulizi lingine lilitokea katika kituo cha kuzalisha umeme cha al-Debis, kilomita 35 kaskazini mashariki ya Kirkuk, na kusababisha vifo vya watu watano na wengine wanne kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako