• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lewis Hamilton ashinda mbio za U.S Grand Prix

    (GMT+08:00) 2016-10-24 10:09:52
    Lewis Hamilton amepunguza pengo alilonalo la pointi zake za ushindi dhidi ya Nico Rosberg baada ya kupata ushindi mnono kwenye U.S Grand Prix.

    Huu ni ushindi wa kwanza kwa Hamilton tangu ashiriki mbio za Grand Prix za Ujerumani mwezi Julai na kumfanya awe nyuma ya mshindani wake wa timu moja ya Mercedes kwa pointi 26. Rosberg amemaliza nafasi ya pili baada ya kurejea kwenye nafasi hiyo alipopitwa na dereva wa Red Bull Daniel Ricciardo mwanzoni mwa mbio hizo. Muaustralia huyo amemaliza nafasi ya tatu akifuatiwa na dereva wa Ferrari Sebastian Vettel. Bingwa wa dunia Hamilton sasa ameshinda mbio 50, wakati ambapo Alain Prost alishinda 51 na Michael Schumacher mbio 91ambaye ameshinda mbio nyingi zaidi katika historia yam bio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako