Mradi wa kilimo cha unyunyizaji maji wa Galana Kulalu uliofikia asilimia 70 kukamilika unatarajiwa kupunguza makali ya baa la njaa yanayoshuhudiwa Kilifi na sehemu nyingine Kenya.
Mhandisi mkuu wa mradi huo Henry Ochiere amesema ekari elfu 10 za ardhi zitapandwa mahindi kutumia kilimo cha unyunyizaji kuanzia machi mwakani.
Katika awamu ya kwanza ,ekari 600 za mahindi zitapandwa katika mda wa siku saba ambapo mbegu ya aina saba ya mahindi itapanda ili kuboresha mavuno.
Kilimo hicho kitatumia mbinu ya kuhifadhi maji kutoka mto Tana ili kuzalisha chakula kwa wengi.
Bodi ya kitaifa ya unyunyizaji maji imepiga kambi kwenye eneo la Tana River ili kuendeleza utafiti wa mradi huu.
Wakaazi wa Tana River tayari wanavuna chakula kingi cha biashara na matumizi mwaka huu baada ya serikali ya Israel kushirikiana na wizara ya kilimo ya Kenya kwa ujuzi wa kilimo hichi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |