Shirika la kimataifa la ulinzi wa wanyamapori WWF limeonya katika ripoti mpya kuwa idadi ya wanyama pori duniani itapungua kwa theluthi mbili hadi kufikia mwaka 2020, kutokana na vitendo vya binadamu. Ripoti hiyo inasema idadi ya samaki, ndege, wanyama, amfibia na wataambazi imepungua kwa asilimia 58 kati ya mwaka 1970 na mwaka 2012. Ripoti imesema tishio kwa uwepo wa viumbe linatokana moja kwa moja na shughuli za binadamu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |