• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la FBI latangaza kuanzisha tena uchunguzi wa "tukio la barua pepe" la Hillary

    (GMT+08:00) 2016-10-29 18:30:05

    Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani FBI Bw. James Comey ameliandikia barua bunge la taifa akilitaarifu kuanzisha tena uchunguzi kuhusu suala la mgombea urais wa chama cha Democratic Bibi Hillary Clinton aliyetumia huduma binafsi ya mtandao kushughulikia barua pepe za siri wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

    Barua hiyo imesema, katika uchunguzi mwingine usiohusiana na Bibi Hillary, shirika la FBI liligundua barua pepe mpya zinazo onekana kuhusishwa na tukio la barua pepe la Hillary. Hivi sasa FBI inatathmini barua pepe hizo. Lakini Bw. Comey hakutaja yaliyomo kwenye barua hizo wala kudokeza watumaji na wapokeaji wa barua hizo.

    Mgombea urais wa chama cha Republican Bw. Donald Trump katika mkutano wa kampeni za kugombea urais uliofanyika jimboni New Hampshire ameshambulia ufisadi wa Hillary kutokana na tukio lake la barua pepe, huku akilaumu kuwa Bi Hillary hastahili kugombea urais.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako