• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mueritrea Ghilagab na Muethiopia Zeleke washinda mbio za marathoni China

    (GMT+08:00) 2016-10-30 18:24:38
    Wanariadha Kaleab Ghilagabr wa Eritrea na Habtewold Zekele kutoka Ethiopia wameshinda mbio za marathoni za kimataifa za Changsha 2016 kwa upande wa wanaume na wanawake zilizofanyika leo katika mkoa wa Hunan China.

    Ghilagabr amekimbia kwa saa 2 dakika 15 na sekunde 2, akifuatiwa na Bellor Yator wa Kenya na Kenenisa Hirpha toka Ethiopia aliyeshika nafasi ya 3.

    Katika mbio za wanawake, Muethiopia Habtewold ameshinda kwa kutumia saa 2, dakika 37 na sekunde 29 akifuatiwa na Getachew Debebe na Urge Soboka.

    Washindi hao watazawadiwa kiasi cha dola 8,000 za kimarekani.

    Mashindano ya kimataifa ya marathoni ya Changsha yalizinduliwa mwaka 2015 na kujumuisha mbio ndefu, mbio za kati na mbio fupi. Jumla ya wanariadha 20,000 pamoja na waalikwa 14 wameshiriki mashindano ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako