• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa mchango mkubwa zaidi katika masuala ya haki za binadamu duniani

    (GMT+08:00) 2016-10-31 21:12:27

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, China itatumia fursa ya kuendelea kuwa mwanachama wa Baraza la Haki za Binadamu, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika masuala ya haki za binadamu duniani.

    China imepata kura 180 katika Baraza Kuu la 71 la Umoja wa Mataifa na kuendelea kuwa nchi mwanachama wa Baraza la haki za binadamu kati ya mwaka 2017 na 2019, ikiwa ni mara ya nne kwa China kuwa nchi mwanachama katika baraza hilo tangu lianzishwe.

    Bibi Hua Chunying ameongeza kuwa, China itaendelea kushiriki kwenye usimamizi wa masuala ya haki za binadamu duniani, kutekeleza kwa makini wajibu wake wa kimataifa, na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano na nchi za nje katika masuala ya haki za binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako