• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Barawai wa Ulaya anaweza kuruka kwa miezi 10 mfululizo!

  (GMT+08:00) 2016-11-01 10:50:28

  Mnandi pwani anayeweza kuruka kwa miezi miwili mfululizo aliwahi kuchukuliwa kuwa ndege mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kuruka. Lakini baadaye watu waligundua kuwa barawai mwenye tumbe jeupe (alpine swift) anaweza kuruka kwa miezi 6 mfululizo. Sasa rekodi hii imevujwa na barawai wa Ulaya.

  Prof. Anders Hedenstrom wa Chuo Kikuu cha Lund cha Sweden amegundua kuwa Barawai wa Ulaya wanatua kwenye nchi kavu kwa miezi miwili tu kila mwaka ili kuzaliana, baadaye wanaelekea Afrika wakitokea Ulaya ili kupisha majira ya baridi, halafu wanarudi tena Ulaya kwa ajili ya kuzaliana. Katika kipindi cha miezi 10 wanapohama, kimsingi hawatui.

  Prof. Hedenstrom na wenzake wameweka vifaa vidogo vya kurekodi data kwa barawai 13 waliokamatwa kusini mwa Sweden, na kuchunguza hali yao kwa miezi miwili.

  Matokeo yanaonesha kuwa ingawa barawai wachache waliwahi kutua kwa muda mfupi wakati wa usiku, au kulala kwa usiku mzima katika majira ya baridi, lakini muda huo haujafikia asilimia 1 ya kipindi cha miezi 10. Na barawai wengine hawakuwahi kutua walipohama na kupisha majira ya baridi.

  Basi ndege hao wanawezaje kulala? Profesa Hedenstrom alisema anakadiria kuwa ndege hao huenda wanaweza kulala huku wakiruka kama mnandi pwani wanavyofanya.

  Unaweza kufikiria kuwa ndege hao wanaishi maisha magumu kwa sababu wanaruka kwa muda mrefu sana, lakini ndege hao wana umri mrefu. Barawai mwenye umri mkubwa zaidi aliishi kwa miaka 20. Profesa Hedenstrom alisema umbali anaosafiri ndege mwenye umri huo ni sawa na kwenda mwezini na kurudi duniani mara 7.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako