Li anatarajiwa kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Kyrgyzstan Sooronbay Jeenbekov, na kukutana na rais wa nchi hiyo Almazbek Atambayev ili kubadilishana maoni kuhusu uhusiano na ushirikiano wa nchi hizo mbili kwenye sekta za uchumi, usalama, utamaduni na maeneo mengine. Mazungumzo hayo pia yatazingatia pendekezo la China la Ukanda Mmoja na Njia Moja, ambalo linajumuisha Njia ya Hariri ya Uchumi na Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21.
Nchi hizo mbili zitasaini taarifa ya pamoja na makubaliano mengine kwenye sekta mbalimabli, kama vile uchumi na biashara, uwezo wa uzalishaji, usafiri, kilimo, na haki miliki ya ubunifu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |