Inter kwa sasa wapo nafasi ya 12 Serie A baada ya kushindwa 1-0 Sampdoria juzi Jumapili. Hiyo ilikuwa mechi yao ya nne kushindwa katika mechi tano za ligi walizocheza chini yake msimu huu.
De Boer mwenye miaka 46, alikuwa beki wa Uholanzi enzi za uchezaji wake na aliwahi kuwa mkufunzi wa Ajax. Alihusishwa na kuhamia klabu za Everton na Southampton majira ya joto.
Inter leo watakutana na Southampton ligi ndogo ya Ulaya, Europa League. Mkufunzi wa timu ya vijana Stefano Vecchi atakuwa kwenye usukani mechi hiyo. Wakati wa uchezaji wake, alichezea Ajax, Barcelona, Galatasaray na Rangers.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |