• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya Misri yaruhusu mabadiliko huru ya kiwango cha ubadilishaji wa fedha

    (GMT+08:00) 2016-11-04 09:55:16

    Benki kuu ya Misri imetangaza kuruhusu mabadiliko huru ya kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya Misri, ili kuondoa matatizo ya kiuchumi na kutekeleza ahadi kuhusu mikopo kati yake na Shirika la fedha la kimataifa IMF.

    Baada ya uamuzi huo kutolewa, kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya Misri kwa dola za kimarekani kimepungua kwa asilimia 48.

    Mwezi Machi mwaka huu kutokana na upungufu wa akiba ya fedha za kigeni, na kuongezeka kwa kiasi cha ubadilishaji wa dola za kimarekani katika soko haramu, benki kuu ya Misri ilitangaza kutekeleza sera nyumbufu ya kiwango cha ubadilishaji wa fedha, na kiasi cha ubadilishaji kati ya sarafu ya Misri na dola za kimarekani kilipungua kwa kiasi kikubwa baada ya kutolewa kwa sera hiyo.

    Wachambuzi wanaona kuwa kupungua kwa thamani ya fedha za Misri kunaweza kuhakikisha usalama wa mfumo wa fedha nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako