• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yamaliza utengenezaji wa darubini ya anga ya juu ya James Webb

  (GMT+08:00) 2016-11-04 15:57:39

  Baada ya kufanya kazi kwa miaka 20, shirika la anga ya juu la Marekani NASA limemaliza utengenezaji wa darubini ya anga ya juu ya James Webb ambayo ni darubini kubwa zaidi ya anga ya juu duniani na ni mrithi wa darubini ya Hubble.

  Sehemu kuu ya darubini hiyo yenye kipenyo cha mita 6.5 inaundwa na vioo 18 vya manjano vyenye umbo la pembesita. NASA itaifanyia majaribio mbalimbali, halafu itaiweka kwenye mwavuli wa kukinga jua wenye ukubwa wa kiwanja cha tenisi. Kwa mujibu wa mpango, darubini hiyo itarushwa angani kwa roketi ya Ariane 5 katika kituo cha safari ya anga ya juu huko French Guiana mwezi Oktoba mwaka 2018.

  Mwanasayansi mwandamizi wa mradi wa darubini hiyo Bw. John Mather alisema darubini ya James Webb ina uwezo mkubwa zaidi kuliko darubini ya Hubble, kwa sababu ukubwa wa vioo vya darubini ya James Webb ni mara 6 ya ule wa Hubble, na tofauti na Hubble, James Webb inaweza kupokea mawimbi yanayokaribia mwanga wa infrared, na kufanya kazi katika mazingira yenye joto karibu na nyuzi 273.15 chini ya sifuri.

  Licha ya NASA, shirika la anga ya juu la Ulaya ESA na shirika la anga ya juu la Canada CSA pia yameshiriki kwenye utengenezaji wa darubini hiyo ambayo imegharamu dola za kimarekani bilioni 8.7.

  Darubini ya Hubble ilirushwa angani mwaka 1990, kwa mujibu wa mpango, itaendelea kufanya kazi mpaka mwaka 2021.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako