• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika zinashirikiana kwenye ulinzi wa ziwa la maji baridi

    (GMT+08:00) 2016-11-06 18:04:46

    Ziwa Poyang na Ziwa Victoria, maziwa makubwa zaidi ya maji baridi katika nchi ya China na bara la Afrika mtawalia yanalenga kushirikiana zaidi kwenye ulinzi wa mazingira na maendeleo.

    Chen Kui, mtaalamu wa ikolojia ya ziwawa Kamati kuhusu maendeleo na ulinzi wa milima, mito na maziwa mkoani Jiangxi, China amesema watafiti wa China wamekamilisha utafiti kuhusu Ziwa Victoria na kubadilishana maoni na idara za serikali, taasisi za kitaaluma na asasi za kiraia za huko kuhusu maendeleo na mazingira ya ziwa hilo.

    Naye Mkurugenzi wa ofisi mtendaji wa Kamati hiyo Dai Xingzhao ameitikia kauli za Bibi Chen akisema Ziwa Poyang pia linakabiliwa na changamoto zinazofanana katika miongo kadhaa iliyopita haswa katika kushughulikia na kuzuia ardhi kuwa jangwa na kurudisha mazingira mazuri. Ameongeza kuwa China na Afrika zinahitaji kushirikiana kwenye kutafuta maendeleo ya kiuchumi na kulinda mazingira na kwamba nguvu za kubadilishana ujuzi na uzoefu kati ya pande hizo mbili ni kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako