• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuwa na kilowati milioni 58 za umeme wa nyuklia ifikapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2016-11-07 19:49:50

    China inatarajiwa kuwa na kilowati milioni 58 za umeme unaotokana na nguvu ya nyuklia itakapofika mwaka 2020, ikiwa ni jitihada za nchi hiyo kupanua mtandao wa nishati safi na ukuaji wa uchumi usiochafua mazingira.

    Mpango wa 13 wa miaka mitano kuhusu maendeleo ya nishati uliotolewa na Idara ya Usimamizi wa Nishati na Kamati ya Mageuzi na Maendeleo ya China umesema, tayari serikali ina kituo cha kuzalisha karibu kilowati milioni 30 za nishati ya nyuklia kitakachoanza kufanya kazi, na vituo vingine kama hivyo vitajengwa katika miaka mitano ijayo.

    Nishati ya kisukuku itachukua nafasi kubwa zaidi kwa kuwa serikali inalenga kuinua matumizi yake ya jumla ya nishati na kufikia asilimia 15 itakapofika mwisho wa mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako