• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuna roketi gani kubwa duniani?

  (GMT+08:00) 2016-11-08 15:32:14

  Roketi mpya ya China Long March 5 ilirushwa kwa mafanikio tarehe 3. Roketi hii ni kubwa zaidi kuliko roketi zilizopita za Long March, ambayo ina kipenyo cha mita 5 na urefu wa mita 57, na nguvu yake pia ni mkubwa zaidi, ambayo inaweza kusafirisha tani 25 za mizigo kwenda mzingo wa chini unaozunguka dunia LEO na tani 10 kwenye mzingo wa juu unaozunguka dunia GTO.

  Roketi kubwa zenye uwezo unaofanana na roketi ya Long March 5 ni kama zifuatazo:

  1. Roketi ya Ariane 5

  Roketi hii iliyotengenezwa na Ulaya ilirushwa mwaka 1996 kwa mara ya kwanza. Ina urefu wa mita 50.5 na kipenyo cha mita 5.4. Inaweza kusafirisha tani 10 kwenda mzingo wa juu wa dunia na tani 20 kwenda mzingo wa chini.

  2.Roketi ya Angara A5

  Roketi hii iliyotengenezwa na Russia ilirushwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014. Ina urefu wa mita 55 na uzito wa tani 750. Inaweza kusafirisha tani 25 kwenda mzingo wa chini wa dunia na tani 7 kwenda mzingo wa juu.

  3. Roketi ya Atlas V

  Roketi hii iliyotengenezwa na kampuni ya ULA ya Marekani, inaweza kubeba tani 8.9 kwenda mzingo wa juu wa dunia na tani 18.85 kwenda mzingo wa chini.

  4. Roketi ya Delta IV

  Roketi hii ilitengenezwa na Marekani kwa lengo la kubana gharama ya utengenezaji. Roketi hii inaweza kupeleka tani 11 kwenda mzingo wa juu wa dunia na tani 25 kwenda mzingo wa chini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako