• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ukitaka kula nyanya zinazonukia, usiweke kwenye friji

  (GMT+08:00) 2016-11-08 15:32:32

  Nyanya ni mboga inayopendwa na watu wengi, kwa sababu inapatikana kwa urahisi sokoni, inaweza kuhifadhiwa kwa siku nyingi, na kupika nyanya kunahitaji dakika chache tu. Lakini baadhi ya watu wanalalamika kwamba nyanya hazinukii kama siku za nyuma. Ni kweli nyanya zinazozalishwa siku hizi ni tofauti na za zamani?

  Ukweli ni kwamba harufu ya nyanya inaathiriwa na baridi. Nyanya zisizowahi kuwekwa kwenye friji, huwa na harufu ya kupendeza zaidi.

  Watafiti wamepima kiasi cha kemikali mbalimbali za nyanya. Matokeo yanaonesha kuwa baada ya kuwekwa kwenye friji, kemikali zinazohusika na harufu zinapungua kwa kiasi kikubwa, lakini kemikali zinazoleta ladha ya utamu zikiwemo glucose na fructose, na zile za asidi zikiwemo malic acid, citric acid huwa hazipungui. Hii inamaanisha kuwa ukiiweka nyanya kwenye friji, ladha haitabadilika, ila tu mharufu yake itapungua.

  Baada ya kupima jeni 25,879 kwenye seli za nyanya, watafiti pia wamegundua kuwa katika mazingira ya baridi, jeni nyingi huwa hazifanyi kazi kama kawaida, ikiwemo jeni zinazohusiana na utoaji wa kemikali zenye harufu. Na hata wakitoa nyanya kwenye friji baada ya kuweka huko kwa siku 8, uwezo wa jeni zinazohusiana na harufu huwa haurudi. Jeni hizi zinaathiriwa hata nyanya zikiwekwa kwenye friji kwa siku moja tu.

  Lakini utafiti huo haumaanishi kwamba huwezi kuweka nyanya kwenye friji, kwani kupoteza harufu ni bora zaidi kuliko kuoza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako