• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kwa nini nyoka hawana miguu

  (GMT+08:00) 2016-11-09 10:36:27

  Dr. Axel Visel kutoka Chuo Kikuu cha California na wenzake wamegundua base pairs 17 kwenye DNA zinahusiana na kuwepo kwa miguu.

  Wanasayansi wamegundua kwamba jeni iitwayo "Sonic hedgehog" ni muhimu sana kwa ukuaji wa miguu wa vinitete vya wanyama wenye uti wa migongo akiwemo binadamu. Karibu na jeni hii, kuna mifululizo mingi maalum ya base pairs ambayo inaweza kuungana na protini maalum na kuihimiza jeni hiyo kufanya kazi. Mfululizo mmoja unaitwa ZRS. Mabadiliko yoyote ya ZRS huenda yakaleta ulemavu, hata mabadiliko ya base pair moja huenda yakasababisha mtoto mchanga kuwa na vidole vingi kuliko kawaida.

  Kikundi cha Dr. Visel kilifanya majaribio ya kubadilisha ZRS za panya kwa kutumia ZRS za wanyama wengine, halafu kuchunguza kama ZRS hizi zinafanya kazi kama kawaida kwenye miili ya panya au la.

  Matokeo yanaonesha kuwa ZRS za binadamu, kuku na samaki zinafanya kazi, lakini miongoni mwa ZRS za aina 6 za nyoka, ni chatu aina ya Boidae tu inafanya kazi. Je, kutofanya kazi kwa ZRS kumesababisha nyoka kupotea miguu?

  Ili kutafuta jibu la swali hili, kikundi hiki kilizalisha vinitete vya panya visivyo na ZRS kwa kutumia teknolojia ya kurekebisha jeni, na kuweka ZRS za binadamu, panya, samaki, chatu aina ya Python na nyoka aina ya king cobra kwenye vinitete hivi, halafu kuchunguza ukuaji wa vinitete. Baada ya siku 18, waligundua miguu haikukua kwenye vinitete vyenye ZRS za nyoka.

  Baada ya kulinganisha jeni za wanyama mbalimbali kwa makini, mwishowe watafiti waligundua kuwa base pairs 17 hazikuwepo kwenye ZRS za nyota. Waliweka base pairs hizi kwenye vinitete vya panya visivyo na miguu, na miguu ilianza kukua tena baada ya wiki mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako