• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanya biashara wa China nchini Kenya watoa shilingi milioni 3.7 kuunga mkono shughuli ya kuhifadhi mazingira na wanyama pori

    (GMT+08:00) 2016-11-11 10:38:17

    Shirikisho la wachina wanaofanya biashara nchini kenya wametoa shilingi milioni 3.7 kwa shirika la kuhudumia wanyampori nchini kenya ili kusaidia kutoa mafunzo kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na wanyama pori.

    Pesa hizo zitatumika kwanza kukarabati jumba la makavazi ya makao makuu ya KWS na pia kufadhili safari za wanafunzi kutoka shule za jamii maskini kuja kutembelea hifadhi ya wanyama ya Nairobi.

    China na Kenya kwa miaka mingi wameshirikiana Kenya katika miradi ya maendeleo na kuhifadhi wanyamapori.

    Chama cha wafanyibiashara wa China na Serikali ya China washirikiana pamoja katika kulinda wanyamapori nchini Kenya kwa kutoa misaada kadhaa kuweza kulinda wanyamapori nchini Kenya.

    China imechangia pakubwa katika kulinda wanyamapori nchini Kenya, na ya baadhi ambayo imetoa ni fedha.

    Bwana Yang Dong ni mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara wa China nchini Kenya, na anaeleza jinsi wanafurahia kuchangia katika kulinda wanyamapori , na kutoa mafunzo kwa jamii kuhusu wanyamapori.

    "Tunafurahi sana kuwasilisha machango wetu kwa ajili ya kutoa mafunzo kuhusu wanyampori kwa jamii, na pia tunatama kama tungechangia katika kujenga kesho bora ya maisha ya wanyamapori kenya"

    mkurugenzi mkuu wa shirika la wanyamapori nchini Kenya bw Kiliti Mbathi, anashukuru juhudi China imeweka katika kulinda wanyamapori nchini Kenya.

    "Ahsante sana kwa kuja kujiunga nasi leo. Bwana balozi umetuunga mkono sana katika kutetea haki za wanyama wetu wa porini. Tungependa sana kupongeza hatua ambayo serikali ya Uchina imechukua, kwa kutangaza rasmi kwamba watafunga masoko yote ya kuuza na kununua pembe za ndovu na vifaru. Kwa sisi Kenya hii ni muhimu sana kwa sababu tunapigana vita vikali dhidi ya wawindaji haramu kwenye mbuga zetu. Lakini endapo masoko yatazidi kuwepo, basi uwindaji haramu utaendelea".

    Balonzi wa china Liu Xianfa alipongeza sana hatua iliyochukuliwa na chama cha wafanyibiashara wa China nchini Kenya, kutoa usaidizi wao katika kulinda wanyamapori.

    Anasema hatua hii inaonyesha ushirikiano mzuri katika ya Kenya na China katika kudumisha biashara na mambo ya kijamii.

    "Inanipa furaha kubwa kuhudhuria sherehe ya kutia saini kati ya shirika la wanyamapori na chama cha wafanyibiashara wa China nchini kenya kwa lengo la kukuza na kubadilishana mawaidha ya kibiashara kati vijana wa China na afrika"

    Anaendelea kusema mradi huu, utatoa usaidizi kwa watoto 500, ambayo ni wadaraja ya chini.

    Sauti ya balonzi wa china Liu Xianfa

    "mpango huu pia utasaidia watoto 500 ambayo wanatoka kwa familia ambazo hazijiwezi, kuweza kupata safari za kielimu ili kukuza mazingira bora ya wanyamapori na kujenga uelewa miongoni mwa vijana nchini na pia kwa jamii ya kichina"

    China kwa upande mwengine imetoa vifaa vyenye thamani ya sh milioni 6 katika shirika la wanyamapori (KWS) kwa ajili ya kudumisha ulinzi wa wanyamapori.

    Sauti ya balonzi wa china Liu Xianfa

    "China ilipeana vifaa vyenye thamani ya sh millioni 6 katika shirika la wanyamapori kwa ajili ya kupiga jeki ulinzi wa wanyamapori"

    Aidha anasema katika mradi wa SGR, China imejali maslahi ya wanyampori kwa kuwajengea njia za kupita.

    Sauti ya balonzi wa china Liu Xianfa

    "Katika mradi wa kilo mita 480 wa SGR njia 14 na daraja 61 zilijengwa kama njia za wanyama kupita"

    Mbunga za wanyampori nchini Kenya zimebakia kuwa kivuti kikubwa kwa wegeni wanao ingia nchini.

    Hivi sasa kuna mbunga 22 za wanyamapori, nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako