• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Popo asiye na mkia wa Brazil ni mnyama anayeruka sambamba na upeo wa macho kwa kasi zaidi

  (GMT+08:00) 2016-11-15 09:05:12

  Ndege wana uwezo mkubwa wa kuruka. Kwa mfano, mwendo kasi wa kuruka chini kwa kipanga aina ya peregrine ni zaidi ya kilomita 300 kwa saa, na mwendo kasi huo wa ndege mvumaji ambaye ni ndege mdogo zaidi duniani ni kilomita 97.2 kwa saa. Katika siku zilizopita, watu walidhani ndege anayeruka sambamba na upeo wa macho kwa kasi zaidi ni barawai wa Ulaya, ambao mwendo kasi wake unaweza kufikia kilomita 111.6 kwa saa. Lakini hivi karibuni wanasayansi wamegundua kuwa rekodi hii imevunjwa na popo asiye na mkia wa Brazil, ambaye anaweza kuruka kwa kilomita 160 kwa saa.

  Ndege wenye mabawa marefu na membamba huruka kwa kasi zaidi kuliko wale wenye mabawa mafupi na mapana. Hivyo watafiti kutoka taasisi ya Max Planck ya Ujerumani waliamua kutafiti popo asiye na mkia wa Brazil. Wameweka vyombo vinavyotoa ishara ya radio kwenye miili ya popo hao, na kuchunguza mwendo kasi wa popo.

  Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa popo jike wenye uzito wa gramu 11 hadi 12 wanaweza kuruka kwa mwendo kasi zaidi ya kilomita 160 kwa saa. Mtafiti Kamran Safri alisema matokeo hayo yamewashangaza, lakini kweli ni sahihi kabisa.

  Utafiti huo umetolewa kwenye gazeti la Royal Society Open Science.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako