• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: waendeshaji Boda Boda watoa wito kwa mahakama kuwaruhusu kufanyakazi katikati mwa jiji

    (GMT+08:00) 2016-11-16 21:14:11

    Wafanyibiashara wa pikipiki maarufu kama bodaboda mjini Nairobi wametoa wito dhidi ya uamuzi wa mahakama kuwazuia wasiingie katikati mwa jiji.

    Mwenyekiti wa chama cha bodaboda Ken Onyango, anasema waendeshaji pikipiki wanadai nafasi mbadala,huku wakibainisha kuwa nchi imekuwa ikitengeneza mapato kutoka kwao.

    Hii ni baada ya Katibu wa kaunti Robert Ayisi kuwapa muda wa wiki mbili kuondoka katikati mwa jiji.

    Aidha anasema kuwa kanuni mpya ya usafirishaji inahitaji kaunti, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Taifa ya Usafiri (NTSA) kuweka eneo la watu bodaboda kuendesha shughuli zao.

    Hata hivyo bw Onyango alilalamika kuwa maofisa wa jiji wamekuwa kuwakamata licha ya kulipia Sh3000 kwa pikipiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako