• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za Afrika waahidi kuchukua hatua za kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2016-11-17 09:01:39

    Viongozi wa nchi za Afrika wametoa ahadi ya kuchukua hatua za kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa na kutekeleza sera zitakazosaidia kuhimiza mabadiliko ya kiuchumi na ya muundo wa kijamii.

    Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano uliofanyika Marrakesh, Morocco ambao ulihudhuriwa na wakuu wa ujumbe kutoka nchi 50 za Afrika, inaahidi kuimarisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Pia wamejadiliana kutekeleza kwa pamoja mikakati ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, inayohusiana na kilimo, usalama, na maendeleo vijijini.

    Kwenye mkutano huo pia imetolewa ramani inayoonesha mpango wa kukabiliana na upanuzi wa jangwa, unaoitwa ukuta mkuu wa kijani. Ukuta huo unahusu eneo litakalopandwa miti lenye urefu wa kilometa 7,700 linalopita kwenye nchi 11, kutoka Senegal hadi Djibouti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako