Gerrard, 36, anaondoka klabu ya LA Galaxy ya New York ambayo hucheza ligi ya MLS. Lawrenson, anapendekeza Gerrard 'kujiunga na timu ya Liverpool' na kutumiwa kama mkufunzi katika timu hiyo.
Amesema litakuwa jambo muhimu kumuweka mchezaji huyo karibu na klabu hiyo, kwa sababu hatachukuliwa kama tishio na Klopp akiwa kwenye benchi la kiufundi. Gerrard alitumikia kwa muda kama mkufunzi wa timu ya Liverpool ya vijana wenye umri chini ya miaka 16 mwaka 2015 na aliifurahia kazi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |