• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viumbe havikuwepo kwenye sayari ya Mars kutokana na ukame mkubwa?

    (GMT+08:00) 2016-11-17 14:53:22

    Uchunguzi kuhusu madini na jiografia ya sayari ya Mars unaonesha kuwa katika zama za kale sayari hii ilifanana na dunia yetu na ilikuwa na maji mengi. Je, viumbe viliwahi kuishi kwenye Mars? Na sasa bado kuna viumbe vinavyoishi kwenye sayari hiyo yenye ukame mkubwa?

    Utafiti mpya uliotolewa kwenye gazeti la Nature Communications unasema ukame mkubwa umekomesha maisha yote na kuifanya Mars iwe sayari yenye mazingira mabaya.

    Katika miaka bilioni 3 iliyopita, Mars ilikuwa na bahari, mito na maziwa na inafaa kwa maisha ya viumbe, lakini sasa imebadilika kuwa sayari yenye ardhi nyekundu.

    Kikundi cha wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Stirling huko Scottland kimetafiti mazingira ya hivi sasa ya Mars. Kiongozi wa kikundi hiki Dr. Christian Shroder alisema hivi sasa tukitaka kutafuta dalili ya viumbe kwenye sayari hii, tunatakiwa kutafuta mapango yenye kina kirefu ambayo yako mbali na ukame na mionzi.

    Kikundi hiki kimetafiti muda wa madini ya chuma kupata kutu kwenye Mars. Muda huo unahusiana na kuwepo kwa maji. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa muda huo kwenye Mars ni mara 10 hadi 10000 ya muda huo kwenye jangwa lenye ukame mkubwa zaidi katika dunia yetu. Hii inamaanisha kuwa ukame umeendelea kwa mamilioni ya miaka kwenye sayari hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako