• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa China wahimizwa na matumizi ya Mtandao wa Internet

  (GMT+08:00) 2016-11-18 09:46:06

  Kwa sasa sikukuu nyingi nchini China zinachukuliwa na wafanyabiashara kama fursa ya biashara, hasa wafanyabiashara wenye maduka kwenye mtandao wa Internet maarufu kama Online shopping.

  Bilioni 10 ndani ya dakika 7

  Tarehe 11 Novemba ambayo inajulikana kama Double 11 nchini China, ni suku ambayo inakuwa na punguzo kuwa la bei kwa maduka mbalimali yanayouza kupitia kwa Internet. Kwenye tovuti ya Taobao pekee, tovuti inayomilikiwa na kampuni ya Alibaba, ambayo ni kampuni mama ya maduka mbalimbali yanayofanya biashara kupitia mtandao wa Internet, thamani ya mauzo ilikuwa zaidi ya dola bilioni 1.47, ndani ya dakika 7 tu baada ya siku hiyo kuanza.

  Hata hivyo kwa mujibu wa mwanzilishi wa Alibaba Bw Jack Ma,, mauzo ya maduka kupitia Internet yanachukua tu asilimia 10 ya mauzo yote ya rejereja nchini China, akimaanisha kuna nafasi kubwa ya maendeleo katika sekta hiyo.

  Uchumi unaotokana na kuenea kwa matumizi ya mtandao wa Internet umechangia sana maendeleo ya uchumi wa China. Takwimu zinaonesha kuwa uchumi wa aina hiyo umechukua asilimia 7 ya GDP ya China. Nido maana kabla ya mkutano wa Mtandao wa Internet duniani kufunguliwa mjini Wuzhen, mashariki mwa China, baadhi ya vyombo vimeripoti kwamba uchumi wa China umeingia kwenye zama ya mtandao wa Internet.

  Wakati Wachina walitumia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 17.6 katika siku ya Double 11 wakisubiri kupokea bidhaa zao, siku nyingine ya punguzo kubwa la bei Desemba 12, yaani "Double 12" inaanza kupiga hodi.

  Internet plus

  Kazi ya Mtandao wa Internet haiishii tu kwenye upande wa uchumi. Sasa sekta mbalimbali nchini China za elimu, huduma na afya zinafuata mkondo wa kuunganika na Mtandao wa Internet, hali ambayo inajulikana kama "Internet plus". Tukichukulia mfano wa huduma za afya, huduma hizo zinapatikana kupitia Internet kufuatia kampuni nyingine kujumuisha madaktari wa idara mbalimbali kujibu maswali kuhusu magonjwa, utapiamlo, malezi ya watoto, matatizo ya kisaikolojia, upunguzaji wa uzito, mazoezi na lishe. Aidha, wananchi wanaweza kupanga mtandaoni kukuta na madaktari, kujiandikisha hospitali kabla ya kwenda mwenyewe hospitali na kujipanga kwenye msururu mrefu, kununua dawa, kutafuta matibabu ng'ambo.

  Zaidi ya hayo, vifaa vinavyovalika na kuunganishwa na simu ya mkononi kama vile saa, bangili, vinawezesha watu kusimamia hali ya afya, ubora wa usingizi na kurekodi mazoezi yaliyofanywa kila siku. Takwimu zinaonesha kuwa thamani ya soko la matibabu kupitia simu za mkononi kwa mwaka jana ilikuwa zaidi ya Dola za kimarekani milioni 612.

  Maisha yalivyo katika zama hii

  Katika zama hii ambayo mtandao wa Internet umepenya katika sekta mbalimbali, maisha nchini China yakoje? Ukimaka wakati badi una uchovu, unatafuta simu kuangalia ulipata usingizi kwa kiasi gani kupitia saa uliyovaa. Ukiwa msalani na simu yako inaita sana, ujue ni habari ulizoagiza zinaibuka kwenye skrini yako. Baadaya kifungua kinywa, unapanda gari la jirani yako anayetumia njia moja na wewe kwenda kazini, kupitia huduma inayopatikana kwenye simu ya mkononi. Ukiwa njiani mnapiga gumzo kuhusu video za kuchekesha mlizoona kwenye mtandao. Baada ya kufika ofisini, hujaketi chini unaitwa kuchukua kifurushi chini, ukishangaa zawadi au bidhaa uliyoagiza jana mtandaoni usiku, inafika asubuhi inayofuata.

  Wakati wa chakula, unakuwa mvivu kula nje kama kawaida, unachukua tena simu kuagiza chakula, hatua ambayo inakuchukulia dakika 20 kutokana na uwepo wa machaguo mengi, muda ambao ungetumia kwenda nje, karibu ungekuwa umekaribia kumaliza chakula. Baada ya nusu saa, chakula kinafika ofisini, unakula huku ukifungua tovuti ambayo inaonesha mechi ya mpira wa kipapu ya ligi ya Marekani NBA moja kwa moja. Unaweza kubadili sehemu ya kamera sababu hii ni huduma kwa mteja anayesajili kwenye tovuti hiyo na kulipa hela. Kazi wakati wa alasiri si nyingi. Kabla ya kutoka kazini unapanga chakula cha jioni na shughuli za usiku. Unanunua mboga na matunda kwa ajili ya chakula cha jioni sababu data za simu zinaonesha kuwa uzito wako umepita kiwango kinachotakiwa siku hizi kutokana na mazoezi machache. Baada ya chakula unaagiza tikiti ya filamu. Ukiwa njiani kwenda sinema, unanunua soda kwenye kiosk na kulipa kwa simu yako, ambapo unaonesha tu QR code kwa mwuzaji., Dunia imebadilika. Kama ingekuwa miaka miwili iliyopita ungehangaika sana kama ukisahahu pochi nyumbani. Kabla ya kulala, unaongea kwa Wechat, APP inayofanana na WhatsApp, na mchumba wako anayeishi mji mwingine na kumwambia unatarajia kumwona wikiendi hii na tayari unamwandalia zawadi, ambayo ni saa kama yako, unamwambia unataka kusikia mapigo ya moyo wake kila wakati.

  Lakini kama basi penzi likizidi unawasha kamera na hapo hapo, na kuanza kuzungumza uso kwa uso na mchumba wako. Haya ndio maisha kwenye zama ya mtando wa internet.

   

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako