• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Marrakesh wafungwa kwa kufikia mpango wa utekelezaji wa Makubalino ya Paris

    (GMT+08:00) 2016-11-19 17:58:07

    Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi COP22 umemalizika mjini Marrakesh kwa kufikia maafikiano juu ya mpango wa utekelezaji wa Makubaliano ya Paris, ambapo washiriki mbalimbali wamesisitiza tena azma zao za kuunga mkono na kutekeleza makubaliano hayo.

    Maamuzi yaliyofikiwa kwenye mkutano huo yanakaribisha nchi zilizoendelea kutoa mpango kuhusu kutoa dola za kimarekani bilioni 100 kila mwaka kabla ya mwaka 2020 ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, na vilevile kuzitaka nchi hizo kuendelea kuongeza pesa hizo, ili kutimiza ahadi zilizozitoa hapo awali.

    Mwenyekiti wa Mkutano wa COP22 ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Morocco Bw. Salaheddine Mezouar ameeleza kuwa kaulimbiu ya mkutano huo ni utekelezaji wa hatua, na pande zote zimetambua udharura wa kukabiliana haraka na mabadiliko ya tabianchi, na zilishiriki kwenye mazungumzo kwa mtazamo wa kuwajibika, hali ambayo ilionesha moyo wa mshikamano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako