• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China awasili Peru kwa ajili ya mkutano wa APEC

    (GMT+08:00) 2016-11-19 18:21:54

    Rais wa China Xi Jinping amewasili nchini Peru kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pacific (APEC) na kufanya ziara yake ya kwanza ya kiserikali nchini humo.

    Mkutano wa APEC umepangwa kufanyika Novemba 19-20 huko Lima, mji mkuu wa nchi hiyo, ukiwa na kauli mbiu ya "Ukuaji Bora na Maendeleo ya Watu", ambapo Xi atatoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kilele wa afisa mkurugenzi mtendaji CEO wa APEC, na kufanya mazungumzo na Baraza la ushauri wa biashara pia kukutana na baadhi ya viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

    China ambayo ni nchi ya pili kwa uchumi duniani imetoa mwito wa kulinda mfumo wa biashara huria duniani na kupinga aina zote za kujilinda kibiashara.

    Baada ya kuhudhuria mkutano huo, Xi atafanya ziara yake ya kwanza ya kiserikali nchini humo, miezi miwili tu baada ya mwenzake wa Peru, Pedro Pablo Kuczynski kufanya ziara nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako