• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi na Obama wakubaliana kudumisha ongezeko zuri na tulivu la uhusiano kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2016-11-20 16:45:22

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Marekani Barack Obama wamekutana leo na kukubaliana kudumisha maendeleo mazuri na tulivu ya uhusiano wa pande hizo mbili.

    Wakikutana pembezoni mwa Mkutano wa Viongozi wa Kiuchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki kwa mwaka 2016 mjini Lima, Xi amepongeza juhudi za rais Obama za kuendeleza uhusiano wa China na Marekani. Xi amesema alikuwa na mazungumzo na Donald Trump baada ya Trump kuchaguliwa na rais ajaye wa Marekani. Amesema anapenda kufanya kazi na Donald Trump ili kupanua ushirikiano kwenye sekta mbalimbali, kudhibiti tofauti kwa njia za kiujenzi na kutambua uhusiano wa aina ya kutopambana, kuheshimiana, ushirikiano wa kunufaishana na kuhimiza zaidi uhusiano kati ya China na Marekani.

    Naye rais Obama amesema yeye na Xi wamejenga uhusiano mzuri, wa kirafiki, kiujenzi, na kuheshimiana. Amemwambia rais Xi kuwa alimsisitizia Trump umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na China na kusema kuna ulazima wa mpito mzuri wa uhusiano wa pande mbili kufuatia uchaguzi wa rais nchini Marekani. Alisema Marekani iko tayari kuendeleza uhusiano endelevu na wenye matunda na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako