• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamthilia za China zaoneshwa kwenye Tamasha la Televisheni la Afrika

    (GMT+08:00) 2016-11-21 16:29:36

    Tamasha la televisheni la Afrika mwaka 2016 limefanyika huko Johannesburg Afrika Kusini.

    Mashirika manane ya China ikiwemo Radio China Kimataifa, kampuni ya video ya kimataifa ya Kituo Kikuu cha Televisheni cha China CCTV, na kampuni ya StarTimes ya Beijing yameshiriki kwenye tamasha hilo. Masharika hayo yamepeleka vipindi vya televisheni zaidi ya 100 vikiwemo tamthilia na filamu zinazoonesha mambo halisi, katuni, na vipindi vya burudani.

    Msimamizi wa kampuni ya Star Times amefahamisha kuwa tamthilia nyingi za China zimetafsiriwa kuwa lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa na Kiyoruba, na kutangazwa katika nchi za Afrika. Amesema tamthilia zinazopendwa na watazamaji wa Afrika ni pamoja na zile zinazohusu kungfu, maisha ya kisasa ya mjini, na maisha ya Wachina barani Afrika au Waafrika nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako