• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Andy Murray atwaa taji la fainali za Dunia za ATP 2016

    (GMT+08:00) 2016-11-22 14:26:23

    Andy Murray amemshinda Novak Djokovic na kufanikiwa kubeba taji la kwanza la fainali za Dunia za ATP 2016 akiwa kama mchezaji namba moja duniani. Akiwa katika kiwango cha juu mwishoni mwa mwaka, Murray ameshinda fainali hizo kwa 6-3 6-4 katika uwanja wa O2 arena mjini London

    Baada ya kukabidhiwa taji lake raia huyo wa Scottland amesisitiza kuwa licha ya kumaliza mwaka akiwa mchezaji bora lakini, anataka kuendeleza kiwango chake, ili mwaka ujao, aendelee kuwa namba moja. Murray, mwenye umri wa miaka 29, amekuwa mchezaji bora katika mashindano 24. Kwa ushindi huo, Murray ameongeza rekodi yake ya kucheza michezo 24 mfululizo bila kupoteza na kuzima ndoto za Djokovic za kutwaa taji hilo kwa mara ya tano mfululizo. Djokovic anabaki kuwa na mataji sita ya michuano hiyo sawa na Roger Federer.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako