• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi apanga mpango mpya wa maendeleo kwa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Latin Amerika

    (GMT+08:00) 2016-11-22 16:15:16

    Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito kwa China na nchi za Latin Amerika kuimarisha mazungumzo kuhusu masuala ya kimataifa na kuongeza ushirikiano kwenye maendeleo ya ndani, ili kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati yao katika kipindi kipya cha mwanzo kwenye historia. Rais Xi amesema hayo akihutubia Bunge la Peru katika ziara yake ya kwanza ya kiserikali nchini humo, baada ya kuhudhuria mkutano wa mwaka wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC mjini Lima.

    Kwenye hotuba yake, rais Xi amesema China na nchi za Latin Amerika zina fursa ya kutafuta nguvu mpya za ukuaji, na kupanua wigo wa ushirikiano ili kupata maendeleo makubwa zaidi. Anasema,  "China na nchi za Latin Amerika na Caribbean zinapaswa kunyanyua bendera ya maendeleo na ushirikiano wa amani, kutafuta uratibu kwenye mikakati yao ya maendeleo, kuongeza kasi na kuinua ngazi ya ushirikiano kivitendo na kuwaletea manufaa watu wa pande hizo mbili."

    Hivi sasa, China ni mwenzi mkubwa wa pili wa kibiashara wa Latin Amerika huku Latin Amerika ikiwa ni eneo ambalo China inawekeza zaidi nje ya nchi baada ya Asia. Rais Xi amesema China inatekeleza mageuzi ya utoaji wa bidhaa na kuharakisha mabadiliko ya njia za kujiendeleza kiuchumi, ambapo soko la China lenye watu bilioni 1.3 lina nguvu zisizohesabiwa, na marekebisho ya muundo wa kiuchumi na maboresho ya kiviwanda vitatoa mahitaji mengi ya bidhaa kwa nje.

    Anasema, "Inakadiriwa kuwa katika miaka mitano ijayo, thamani ya uagizaji bidhaa kutoka nje itafikia dola za kimarekani trilioni 8, mitaji ya kigeni itakayotumiwa nchini China itafikia dola za kimarekani bilioni 600, thamani ya uwekezaji kwa nje itafikia dola za kimarekani bilioni 750 na idadi ya wachina watakaotalii nje itafikia milioni 700. Hayo yote yatatoa soko kubwa, fedha za kutosha, bidhaa za aina mbalimbali na hususan fursa nzuri za ushirikiano kwa nchi mbalimbali duniani. China inakaribisha nchi nyingine kutumia fursa zinazotokana na maendeleo yake ili kujinufaisha kimaendeleo."

    Rais Xi aliwasili Peru Ijumaa iliyopita, ikiwa ni kituo cha pili cha ziara yake ya nchi tatu za Latin Amerika. Alitembelea Ecuador na pia atafanya ziara nchini Chile. Hii ni ziara ya tatu ya Rais Xi kwa Latin Amerika tangu aingine madarakani mwaka 2013.

    Kwenye hotuba yake, Xi pia alifanya majumuisho ya mahusiano na mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Peru, na kati ya China na nchi za Latin Amerika katika miaka iliyopita. Kabla ya hotuba yake, Xi alitunukiwa nishani ya Grand-Cross ya Bunge la Peru na mkuu wa Bunge Bw Luz Salgado.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako