• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNAIDS yasema watu milioni 18.2 wanatumia ARV

    (GMT+08:00) 2016-11-22 18:51:15

    Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa UNAIDS jana nchini Namibia imeonyesha kuwa, watu milioni 18.2 wanatumia dawa za kurefusha maisha (ARV's).

    Takwimu hizo mpya zinamaanisha kuwa watu milioni moja zaidi wanapata tiba katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, kama juhudi zitadumishwa na kuongezwa, dunia itakuwa kwenye mwelekeo sahihi wa kutimiza lengo la watu milioni 30 kupata tiba ifikapo mwaka 2020.

    Ripoti hiyo iliyotolewa kabla ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo huadhmishwa Desemba Mosi, imesema watu wako kwenye hatari ya kupata maambukizi ya UKIMWI katika umri fulani kwenye maisha yao, na imetoa wito wa kufuata mzunguko wa maisha ili kutafuta suluhisho kwa kila mtu katika kila ngazi ya maisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako