• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Licha ya dunia yetu, theluji pia inaanguka kwenye sayari na satilaiti mbalimbali

  (GMT+08:00) 2016-11-23 10:35:36

  Katika dunia yetu, theluji inaanguka wakati wa majira ya baridi. Theluji ni nyeupe na inaundwa na maji. Tukiiangalia dunia kutoka anga ya juu, tutaona ncha mbili za dunia zikifunikwa na theluji.

  Sayari nyekundu ya Mars pia ina ncha nyeupe, ambazo zinamaanisha kuwa theluji inadondoka kwenye sayari hiyo. Lakini Mars ina ukame mkubwa, hivyo theluji ya huko inaundwa na Carbon Dioxide badala ya maji.

  Unadhani theluji yote ni nyeupe? Satilaiti ya Io ya sayari ya Jupiter ina volkeno nyingi. Sulfur dioxide inayeyuka na kurushwa angani na volkeno, halafu inaganda na kuwa theluji ya manjano.

  Kwenye satilaiti ya Triron ya sayari ya Neptune, theluji inaundwa na Nitrogen na Methane. Majimaji ya kemikali hizi yanarushwa angani kupitia chemichemi, na kubadilika kuwa theluji yenye rangi ya waridi. Theluji inaanguka na kufunika ncha ya kusini ya satilaiti hii.

  Na theluji ya rangi ya waridi pia inaanguka kwenye sayari kibeti ya Pluto. Picha zilizopigwa na chombo cha safari ya anga ya juu cha New Horizons zinaonesha kuwa Pluto ina eneo kubwa lenye umbo la moyo. Hili ndilo eneo linalofunikwa na theluji. Theluji ya huko inaundwa na Nitrogen na Methane, na pia huenda ina Carbon monoxide chache.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako