• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua tovuti ya ajira kwenye mtandao wa Internet

    (GMT+08:00) 2016-11-25 08:52:50

    Kenya imezindua tovuti ya ajira kwenye mtandao wa Internet ikiwa ni hatua ya programu itakayonufaisha vijana zaidi ya milioni moja wasio na ajira kwa mwaka kesho.

    Programu hiyo inatarajiwa kuongeza nafasi za ajira kwa wakenya kwa njia ya kutoa vifaa na mafunzo yanayohitajika kuwawezesha vijana wapate ajira na mapato.

    Waziri wa habari na teknolojia ya mawasiliano wa Kenya Bw. Joe Mucheru amesema, programu hiyo inalingana na ahadi ya serikali ya kuongeza nafasi za ajira na pia ni hatua ya kuitikia mwelekeo wa ukuaji wa kasi wa soko la ajira kwenye mtandao wa Internet kote duniani.

    Bw. Mucheru amesema kwa sasa wakenya zaidi ya elfu 40 wanafanya kazi kupitia mtandao wa Internet, na kuifanya Kenya ichukue nafasi ya 10 duniani na nafasi ya kwanza barani Afrika kwa idadi ya wafanyakazi kwenye mtandao wa Internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako