• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cuba yatangaza siku 9 za maombolezo ya taifa kwa Fidel Castro

    (GMT+08:00) 2016-11-27 17:30:05

    Serikali ya Cuba jana imetangaza siku 9 za maombolezo ya taifa, kutokana na kifo cha kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Fidel Castro.

    Fidel Castro alifariki dunia tarehe 25 usiku akiwa na umri wa miaka 90. Viongozi wa nchi mbalimbali duniani wametoa salamu za rambirambi kwa serikali ya Cuba na wananchi wake.

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa rais wa Cuba Raul Castro, akisema kuwa, Fidel Castro ni mtu mashuhuri sana katika zama zetu, atakumbukwa daima katika historia.

    Ikulu ya Marekani ilitoa taarifa ikisema kuwa, historia itarekodi na kutathimini athari ya Fidel kwa watu wa Cuba na dunia nzima.

    Viongozi wa Umoja wa Ulaya pia walitoa taarifa na kutoa salamu za rambirambi kutokana na kifo chake. Taarifa hiyo inasema Umoja wa Ulaya itaendelea kuimarisha uhusiano kati yake na Cuba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako