• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa Samburu waitaka serikali ya Kenya kuongeza bei ya mahindi

    (GMT+08:00) 2016-11-28 09:32:09

    Wakulima wa kutoka kaunti ya Samburu wanatishia kuwachana na kilimo cha mahindi , iwapo serikali kuu na serikali ya kaunti itasusia kuongeza bei ya mahindi na kufika sh 3,500.

    Kutokana na ukame unaoshuhudiwa hivi sasa nchini, wakulima wanalalamikia bei za chini za mazoa, na wengine wa wakulima wakisema hakuna faida wanayo tengeneza licha ya gharama ya uzalishaji kuwa juu.

    Kando na ukame unaoshuhudiwa nchini hivi sasa, wakulima wa samburu wamepanga kususia kilimo mahindi kwa kuwa mapato yake yameenda chini mno ikilinganishwa na hapo awali.

    Wakulima katika kaunti ya samburu wameamini sana kilimo mahindi kwa kuwa ndicho kinaleta chakula

    Ruth ni mkazi wa samburu na anasema wao utegemea kilimo mahindi sana.

    "Ndio januari tunategemea kusomesha watoto wetu , watoto wakienda shule ni hiyo mahindi unategemea"

    Wakulima hapa wanalalamika mapoto zao hilo linaleta.

    Wakulima wanasema licha ya gharama kubwa inayotumika kuzalisha zao hilo, mapato yake niya chini mno.

    Nguni ya kilo 90 ambayo ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 2,500 hivi sasa imeshuka hadi sh 1,800.

    Hivi sasa wakulima hao wanaitaka serikali kuu na serikali ya kaunti kuunga na mkono na kutafuta soko la zao lao.

    Mkulima Loosenge anasema kwamba wanatapeliwa na serikali ya kaunti.

    "Serikali kuu ilisema inanunua na sh 3,500 na serikali ya kaunti imesema inanunua na sh 2,400 hakuna tofauti na wale watapeli"

    Wakulima wanasema serikali ya kaunti imeweka juhudi kidogo sana katika kilimo hicho, kwani wengi wakulima hawana sehemu mahali pakuhifadhi mazao yao baada ya kuvuna, hivyo kuchangia ubora wake kuenda chini.

    Hata hivyo serikali ya kaunti iliwaahidi wakulima kwamba itaweka kamiti kuweza kutafuta fedha za kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

    Afisa mkuu wa kilimo katika kaunti ya Samburu, anasema haya.

    "Mapendekezo yetu ya kwa wakulima ni kununua kutoka kwao na kuweka kwa BODI YA NAFAKA, ilikuweza kununua kwa sh 3,500"

    Bei ya mahindi hadi sasa imebaki sh 2,400 kitu ambacho kinaumiza sana wakulima wasamburu, wengi wakioneka kuacha kilimo hicho na kuingilia kilimo chengine.

    Mwanzoni mwa wiki hii, Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) ilitangaza kwamba itakuwa ikinunua mahindi kutoka vyama vya ushirika ambazo vimesajiliwa kisheria na vikundi vya wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako