• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanamfalme Maha Vajiralongkorn athibitishwa kuwa mfalme mpya wa Thailand

    (GMT+08:00) 2016-11-29 18:20:41

    Bunge la Thailand jana mchana limefanya mkutano maalumu, ambapo spika wa bunge hilo Bw. Pornpetch Wichitcholchai ametangaza kuwa mwanamfalme Maha Vajiralongkorn amethibitishwa rasmi kuwa mfalme mpya wa Thailand.

    Akizungumza katika mkutano huo, Spika Pornpetch amesema serikali ya Thailand ililiarifu bunge kuwa kabla ya kufariki dunia, mfalme Bhumibol Adulyadej alimthibitisha mtoto wake Vajiralongkorn kuwa mrithi wake. Kutokana na katiba na sheria husika nchini Thailand, bunge la Thailand limezindua rasmi utaratibu husika na kumwomba Vajiralongkorn kuwa mfalme mpya.

    Bw. Pornpetch hakueleza mfalme mpya ataapishwa lini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako