• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mmea unakinga vijidudu kwa kuvizuia visipate lishe

    (GMT+08:00) 2016-11-30 09:16:35

    Utafiti mpya unaonesha kuwa mmea unavikinga vijidudu kwa kuvizuia visipate lishe ya sukari.

    Vijidudu vinapoambukiza mimea, vinakula lishe za sukari inayozalishwa na mimea kupitia mchakato wa usanisinuru.

    Watafiti wa Chuo Kikuu cha Kyoto cha Japan wamegundua kuwa kwenye majani ya mmea aina ya "thale cress" kuna protini maalum inayopeleka lishe ya sukari iliyoko nje ya seli kwenda ndani. Wakati mmea huo unapoambukizwa vijidudu, protini hii inafanya kazi zaidi ili kukinga vijidudu. Baada ya protini hiyo kupeleka lishe nyingi zaidi ya sukari ndani ya seli, vijidudu haviwezi kupata lishe ya kutosha na haina uwezo mkubwa wa kuambukiza mmea huo.

    Watafiti wamejaribu kuifanya protini hiyo isifanye kazi, baadaye wamegundua idadi ya vijidudu inaongezeka kwa kiasi kikubwa, na mmea huo unapata magonjwa.

    Watafiti wanaona mimea ya aina nyingi pia ina uwezo huo. Utafiti huo unatazamiwa kuwasaidia wanasayansi kuzalisha dawa za kutibu magonjwa ya mimea. Utafiti huo umetangazwa kwenye tovuti ya gazeti la Sayansi la Marekani.

    Mmea aina ya "thale cress" ni mmea unaotumiwa kwa wingi kwenye utafiti. Mmea huo ni mdogo, una maisha mafupi, unajichavusha na unazaa mbegu nyingi, hivyo unafaa kufanyiwa utafiti wa jeni za mmea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako