Kamanda wa polisi wa Kenya Inspekta Jenerali Joseph Boinnet amesema kundi la Al-shabaab linapanga kukusanya wapiganaji wake katika eneo la Jedahaley nchini Somalia, na kuingia nchini Kenya kufanya mashambulizi kwenye maeneo ya mpakani na sehemu za utalii katika pwani ya Mombasa, wakiwalenga wana usalama na vyombo vya usafiri wa umma.
Imefahimika kuwa baadhi ya wapiganaji wanapanga kujipenyeza kuingia Kenya kwa kujifanya wafugaji. Sehemu za mpakani zimetajwa kuwa na tishio kubwa la usalama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |