• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Swala wa Saiga laki 1.2 walikufa ghafla katika mwezi mmoja

  (GMT+08:00) 2016-12-01 15:46:50

  Watu wengi hawajawahi kusikia jina la swala wa Saiga ambao wana pua kubwa na refu. Idadi yao ni ndogo na inaendelea kupungua. Wao ni jamaa wa karibu wa swala wa Tibet ambao pia wako hatarini.

  Swala wa Saiga waliwahi kuenea katika Ulaya na Asia, lakini swala hawa wanaishi katika nchi za Asia ya Kati na Mongolia tu. Mwishoni mwa karne ya 19, uwindaji wa kupita kiasi uliwafanya kukaribia kutoweka. Katika karne ya 20, idadi ya swala hao ilifufuka, lakini baada ya Urusi kusambaratika, shughuli za uwindaji zilianzishwa tena na swala hao wako hatarini tena. Mwaka 2000 hadi 2002 Shirika la wanyama la Kazakhstan lilifanya uchunguzi kuhusu hali ya swala hao, lakini katika mbuga ya Betpak Dala, wachunguzi hawakuona swala dume hata mmoja. Wawindaji wanawinda swala dume ili kupata pembe zao, na kusababisha kutokuwepo na uwiano kati ya jinsia mbili na kupungua kwa kiwango cha uzazi. Aidha, swala wamehama kutoka makazi yao ya zamani yanayofaa kwa maisha yao, sasa wanaishi katika makundi madogomadogo hapa na pale. Mwezi Mei mwaka 2015, kutokana na maambukizi ya ugonjwa usiojulikana, swala laki 1.2 ambao wanachukua karibu nusu ya swala wote wa Saiga walikufa ghafla.

  Utafiti kuhusu magonjwa ya swala wa Saiga uliwahi kufanyika zamani. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, uwindaji haramu umekuwa suala kubwa zaidi kuliko magonjwa, wafanyakazi wa kulinda wanyama pori wamepuuza suala la magonjwa. Baada ya swala wengi sana kufa ghafla, serikali ya Kazakhstan ilianzisha mradi wa utafiti mara moja ili kuwahifadhi swala hao. Dr. Eleanor J.Milner-Gulland kutoka Uingereza ametafiti swala wa Saiga tangu mwaka 1990, amesema watu wanapohifadhi wanyama pori, si kama tu wanahitaji kutatua matatizo ya dharura, bali pia wanatakiwa kufuatilia hatari zinazoweza kutokea, utafiti wa muda mrefu utasaidia kuelewa vizuri zaidi hatari hizo, na kutunga mikakati kamili ya kuwahifadhi wanyama hao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako