• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majukumu ya kisayansi kuhusu anga ya juu yaliyowekwa katika Mpango ya 13 wa miaka mitano yatekelezwa kwa pande zote

    (GMT+08:00) 2016-12-02 17:09:32

    Taasisi ya sayansi ya China jana tarehe 1 Desemba ilitangaza kuwa, baada ya kurushwa kwa satelaiti mbalimbali za kisayansi katika anga ya juu na kupata mafanikio ya awali ya kisayansi, majukumu ya sayansi katika anga ya juu yaliyowekwa katika Mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano ya China umeanza kutekelezwa kwa pande zote. Taasisi hiyo inasema itafuata mahitaji ya maendeleo ya China katika sekta ya sayansi katika anga ya juu, na kukusanya mapendekezo yanayohusu majukumu ya sayansi katika anga za juu kote nchini.

    Taasisi ya sayansi ya China inasema, hivi sasa majukumu ya sayansi katika anga ya juu yaliyowekwa kwenye Mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano umeanza kutekelezwa kwa pande zote. Naibu mkurugenzi Taasisi hiyo Bw. Xiang Libin amesema satelaiti tano za sayansi zinapagwa kurushwa kabla ya mwaka 2020. Mkurugenzi wa Kituo cha sayansi ya anga za juu cha China Bw. Wu Ji alieleza kuwa, kurushwa kwa satelaiti hizo kunatazamiwa kuchangia kugundua umaalumu wa mabadiliko ya mzunguko wa maji chini ya mabadiliko ya dunia nzima, kanuni ya Space coupling law, uhusiano kati ya sayari ya nguvu ya uvutano ya jua na kimbunga kwenye jua.

    Mbali na kutangaza majukumu ya sayansi wakati wa utekelezaji wa "Mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano", siku hiyo taasisi hiyo pia ilikusanya mapendekezo ya majukumu ya sayansi katika anga ya juu kwa Taasisi za utafiti zinaohusika, vyuo vikuu, na idara za viwanda kote nchini kwa mujibu wa mahitaji ya maendeleo ya sayansi katika anga za juu katika miaka 10 hadi 15 ijayo, ili kufanya maandalizi kwa utafiti na majaribio ya kisayansi katika anga ya juu kwa siku za baadaye. Bw. Wu Ji ameeleza kuwa, mapendekezo hayo yanapaswa kutungwa na wanasayansi wa China, kutupia macho mwelekeo wa sayansi ya kisasa, na kutazamiwa kupata maendeleo makubwa katika sayansi ya kimsingi. Anasemaļ¼š

    "Utekelezaji wa mpango huo unafuata pande mbili, moja ni chimbuko la anga ya juu na vitu, mwingine ni uhusiano kati ya jua na shughuli za binadamu. Tumefanya utafiti juu ya sayansi za kisasa kwa kufuata masuala hayo makuu ya kisayansi."

    Imefahamika kuwa, kazi hiyo ya kukusanya majukumu ya sayansi katika anga ya juu ilianza jana, na baada ya mwezi mmoja, kituo cha sayansi katika anga ya juu cha China kitafanya uchaguzi kati ya mapendekezo yaliyokusanywa. Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya sayansi ya China Bw. Xiang Libin ameeleza kuwa, mapendekezo hayo yataweka msingi kwa miradi ya utafiti wa sayansi ya anga ya juu katika siku zijazo. Anasema:"Baada ya kukusanya mapendekezo hayo, tutafanya majadiliano na kuchagua mapendekezo bora kuwa ajili ya miradi itakayotekelezwa katika Mpango wa 14 au wa 15 wa maendeleo ya miaka mitano."

    Matokeo ya uchaguzi wa mapendekezo hayo yanatazamiwa kutangazwa kabla ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa mwaka kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako