• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 10 tangu Mkataba wa haki za watu wenye ulemavu upitishwe

    (GMT+08:00) 2016-12-03 17:12:11

    Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomesha ubaguzi na kuondoa vikwazo dhidi ya watu wenye ulemavu, na kuwajumuisha vilivyo kwenye mchakato wa kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu.

    Kwenye maadhimisho ya miaka 10 tangu Mkataba wa haki za watu wenye ulemavu upitishwe yaliyofanyika jana, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amesema, mkataba huo unasaidia na kuhimiza maendeleo ya shughuli zinazowahusu watu wenye ulemavu, lakini hivi sasa watu hao hawana nafasi sawa katika kupata elimu, ajira na huduma ya matibabu. Bw. Moon ametaka nchi mbalimbali duniani kuimarisha juhudi na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanashiriki kwa usawa kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.

    Naye mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Peter Thomsen amesema asilimia 80 ya watu wenye ulemavu duniani wanaishi katika umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako