• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanaanga aliyekuwa peke yake alisikia sauti ya ajabu katika anga ya juu

    (GMT+08:00) 2016-12-05 09:10:20

    Kwenye chombo cha anga ya juu ilioyo umbalin wa kilomita 343 kutoka duniani, mwanaanga aliyekuwa peke yake ghafla alisikia sauti inayofanana na kelele za ndoo ya chuma ikipigwa kwa nyundo ya mbao. Kila mara aliposikia sauti hii, alitchungulia nje ya dirisha na kujaribu kutafuta chanzo cha sauti hiyo, lakini alishindwa.

    Mwanaanga huyu ni Bw. Yang Liwei na ni mwanaanga wa kwanza wa China. Wanaanga wengine waliokwenda katika anga ya juu baada ya Bw. Yang pia walisikia sauti hiyohiyo. Na wanaanga wa Marekani waliokwenda kwa chombo cha anga ya juu cha Apollo pia waliripoti kusikia sauti ya ajabu.

    Watu wametoa maoni mbalimbali kuhusu sauti hiyo, hata baadhi ya watu wanasema hiyo ni sauti ya kubisha hodi ya viumbe kutoka nyota nyingine.

    Profesa Liu Hong ambaye ni msanifu wa chombo cha utafiti wa mwezi "Lunar Palace 1" hivi karibuni amefichua sababu ya sauti hii ya ajabu. Alisema watafiti walipofanya majaribio ya chombo hiki mwaka 2013 hadi 2014, waliwahi kusikia sauti hii ya ajabu. Mwishowe waligundua kuwa kutokana na mabadiliko ya joto, shinikizo ndani ya chombo hiki pia lilibadilika, na kusababisha ubao ulioko kwenye ukuta wa ndani kupinda kidogo, na kutoa sauti inayofanana na mipigo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako