• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gabrielle Aroudi Onguene ndie mchezaji bora AWCON 2016

    (GMT+08:00) 2016-12-06 10:40:25

    Kiungo wa Cameroon, Gabrielle Aboudi Onguene ndie mchezaji Bora wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizofikia tamati Jumamosi nchini Cameroon.

    Mabingwa wa mashindano hayo, Nigeria wao wametoa mchezaji Bora Asisat Lamina Oshoala aliyefunga mabao 6, huku wenyeji Cameroon wakishinda na tuzo ya Fair Play.

    Walioteuliwa kwenye kikosi cha AWCON ya mwaka huu, yaani 11 Bora kwa mtiririko wa nafasi uwanajani ni kipa; Annette Ngo Ndom (Cameroon), mabeki; Meffoumetou Tcheno Falone (Cameroon), Osinachi Ohale (Nigeria), Janine Van Wyk (Afrika Kusini) na Linda Eshun (Ghana)

    Viungo ni Jermaine Seoposenwe (Afrika Kusini), Raisa Feudjio Tchuanyo (Cameroon), Elizabeth Addo (Ghana) na Gabrielle Aboudi Onguene (Cameroon) wakati washambuliaji ni Ugochi Desire Oparanozie (Nigeria) na Asisat Lamina Oshoala (Nigeria).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako