• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi ya kamanda wa zamani wa LRA Dominic Ongwen yaanza kusikilizwa The Hague

    (GMT+08:00) 2016-12-07 10:17:01

    Kesi ya kamanda wa zamani wa kundi la Lord Resistance Army LRA, Bw Dominic Ongwen, imeanza kusikilizwa jana huko The Hague, huku mshtakiwa akikana mashtaka dhidi yake.

    Bw Ongwen anakabiliwa na mashtaka ya makosa 70 ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu anaodaiwa kuufanya wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu nchini Uganda. Makosa yake yanahusiana na mashambulizi dhidi ya raia kwenye kambi za Lukodi, Pajule, Odek na Abok kati ya Oktoba 2003 na Juni 2004.

    Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo na baadaye kusikilizwa tena Januari 16.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako